Kusali Rozari Takatifu Matendo Yote 4

Praying the Rosary/ Rozari Takatifu

The purpose of the Rosary is to help keep in memory certain principal events in the history of our salvation. There are twenty mysteries reflected upon in the Rosary, and these are divided into the five Joyful Mysteries (said on Monday and Saturday), the five Luminous Mysteries (said on Thursday), the five Sorrowful Mysteries (said on Tuesday and Friday), and the five Glorious Mysteries (said on Wednesday and Sunday). As an exception, the Joyful Mysteries may be said on Sundays during Advent and Christmas, while the Sorrowful Mysteries may be said on the Sundays of Lent.

  1. Make the Sign of the Cross.
  2. Holding the Crucifix, say the Apostles’ Creed.
  3. On the first bead, say an Our Father.
  4. Say one Hail Mary on each of the next three beads.
  5. Say the Glory Be
  6. For each of the five decades, announce the Mystery (perhaps followed by a brief reading from Scripture) then say the Our Father.
  7. While fingering each of the ten beads of the decade, next say ten Hail Marys while meditating on the Mystery. Then say a Glory Be. (After finishing each decade, some say the following prayer requested by the Blessed Virgin Mary at Fatima: O my Jesus, forgive us our sins, save us from the fires of hell; lead all souls to Heaven, especially those who have most need of your mercy.)
  8. After saying the five decades, say the Hail, Holy Queen, followed by this dialogue and prayer:
    V. Pray for us, O holy Mother of God.
    R. That we may be made worthy of the promises of Christ.
    Let us pray: O God, whose Only Begotten Son, by his life, Death, and Resurrection, has purchased for us the rewards of eternal life, grant, we beseech thee, that while meditating on these mysteries of the most holy Rosary of the Blessed Virgin Mary, we may imitate what they contain and obtain what they promise, through the same Christ our Lord. Amen.

Jinsi Ya Kusali Rozali Takatifu Matendo Ya Utukufu

Rozari Takatifu Matendo Ya Utukufu
Rozari Takatifu

Matendo Ya Rozari Takatifu

MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

Rozari Takatifu Matendo Ya Furaha

Tendo la kwanza

Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu .

Tendo la pili

Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.

Tendo la tatu

Yesu anazaliwa Betlehemu.
Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara

Tendo la nne

Yesu anatolewa hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo .

Tendo la tano

Maria anamkuta Yesu hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.

MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)

Rozari Takatifu Matendo Ya Uchungu

Tendo la kwanza

Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.

Tendo la pili

Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.

Tendo la tatu

Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.

Tendo la nne

Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.

Tendo la tano

Yesu anakufa Msalabani.
Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.

MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)

Rozari Takatifu Matendo Ya utukufu

Tendo la kwanza

Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.

Tendo la pili

Yesu anapaa mbinguni . Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.

Tendo la tatu

Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu .

Tendo la nne

Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.

Tendo la tano

Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema .

MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)

Tendo la kwanza

Yesu anabatizwa Mto Jordani.
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.

Tendo la pili

Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.

Tendo la tatu

Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.

Tendo la nne

Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.

Tendo la tano

Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

Triple Michael
Triple Michael is a gamer and a computer enthusiast who enjoys assisting others by publishing answers to Windows and Android operating system difficulties. In his spare time, he likes watching movies and playing video games.